Dk. Magufuli akiwasalimia wananchi wa Biharamulo (hawapo pichani).
Wakazi wa Biharamulo wakimsikiliza mgombea urais wa CCM, Dk. Magufuli leo.
Wana CCM Biharamulo wakicheza wakati wa mapokezi ya Dk. Magufuli.
Wakazi wa Kakonko mkoani Kigoma wakimkaribisha Magufuli.
Dk. Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni kwenye Kijiji cha Kakonko mkoani Kigoma leo.
Dk. Magufuli akimnadi mgombea wa CCM eneo la Kakonko.
Picha hii imenaswa na mgigapicha wetu eneo la Kakonko, Kigoma.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli leo amemaliza ziara yake mkoani Kigoma kwa kuomba kura katika vijiji vya Kakonko, Kisanda na Buyungu kisha akaingia mkoani Kagera na
kufanya mkutano mkubwa katika Viwanja vya Biharamulo. Baada ya mkutano huo, Dk, Magufuli anatarajia kuingia wilayani Chato mkoani Geita.
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL, BIHARAMULO)