The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Amebaka watoto 11 mmemwachia, mnataka abake wangapi? – VIDEO

RAIS  John Magufuli ameshangazwa na kitendo cha vyombo vya dola kushindwa kumshughulikia mtuhumiwa anayedaiwa kubaka watoto 11 wilayani Mufindi mkoani Iringa na badala yake kumwachia huru kila anapokamatwa na kufikishwa kweye vyombo hivyo.

 

Magufuli amesema hayo leo Jumanne, Januari 29, 2019 wakati akihutubia baada ya kuwaapisha majaji, wakuu wa wilaya na wakurugenzi amabao aliwateua juzi (Jumapili) aliposema mahakama zimekuwa zikipelekewa ushahidi usiojitosheeleza, hivyo kushindwa kufanya maamuzi ipasavyo.

 

“Juzi nilikuwa naangalia TV kule Mufindi, akina mama wanalalamika mbele ya waziri mkuu mstaafu.  Mtu ameshabaka watoto kumi na moja, lakini kila akipelekwa polisi au mahakamani anaachiwa. Na leo ameachWanataka abake watu wangapi ndipo watoe hukumu?” aliuliza rais kwa mshangao akiongeza kwamba katika tukio kama hilo jingine, mtuhumiwa (leo) ameachiwa tena.

 

“Huyu mtuhumiwa amebaka mtoto wa kwanza hadi wa kumi na moja, na anaachiwa;  hivi ushahidi ‘concentrated’ (wenye mashiko) unapelekwa wapi asu mnaletewa ushahidi ‘diluted’ (uliochakachuliwa)?” alisisitiza rais na kusema alikuwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa au Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo mtuhumiwa akamatwe tena na afunguliwe mashtaka upya. 

 

VIDEO: MSIKIE MAGUFULI AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.