The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Hatuchagui Sura, Mchumba Wala Mme – Video

0

MGOMBEA urais Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli, leo Agosti 4, 2020, ameendelea na kampeni za kuwania nafasi hiyo mkoani Simiyu akiomba kura za wananchi na kuwapigia debe madiwani na wabunge wa chama hicho ambapo amesisitiza kwamba waelekeze nadhari yao katika kuchagua watu watakaofanya kazi watakazotumwa si kuendekeza chuki binafsi kwa wagombea hao.

Baadhi ya kauli muhimu alizozitoa Magufuli wilayani Kishapu ni zifuatazo:

“Nafahamu kuna mambo madogo kwamba hamumpendi diwani; usipompenda diwani unakichukia chama.  Hatuchagui mchumba wala mme, tunachagua mtu wa kumtuma kwenda kufanya kazi, kama yapo makosa yake madogo namwombea msamaha, msipomchagua mnanipunguzia nguvu ya kufanya kazi hapa.

 

“Tayari maji tumeshayaleta hapa Kishapu kwa gharama ya Tsh bilioni 15.58, kazi inayofuata ni kuyasambaza katika vijiji mbalimbali, hiyo ni kazi nyepesi, kuingia ndani ni tofauti na kulala kitandani, ukishaingia ndani unaweza kuingia chumba chochote, tuchagueni tukamilishe.

 

“Mmesema kuna eneo lenu hapa Kishapu mnalitaka si ndiyo? Niachieni mimi nitajua cha kufanya, na wewe mbunge hii ndiyo iwe kazi yako ya kwanza kunikumbusha iwapo utachaguliwa, utaniona kama hautofuatilia jambo hili. Nataka siku naapa hii ndiyo iwe kazi ya kwanza.”

Leave A Reply