Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya majaji waliohudhuria hafla ya Siku ya Sheria.Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande akisoma hotuba yake kwa Mgeni Rasmi, Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Hali ilivyokuwa katika hafla hiyo.
Taswira nzima ya hafla hiyo.
Baadhi ya majaji, mahakimu na mawakili wakifuatilia hotuba ya Rais Magufuli iliyokuwa ikiendelea.
Aliyekuwa Kamanda Maalum wa Mkoa wa Kipolisi Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati) akibadilishana mawazo na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza (kushoto) John Casmir Minja, Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar, DCP Simon Sirro ambaye sasa amekalia kiti cha Kova.
Gwaride maalum lililokuwa limeandaliwa.
Majaji wa Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (wa kwanza kulia) kabla ya kukagua gwaride lililokuwa limeandaliwa.
Gwaride likitoa kiapo kwa Jaji Mkuu, Othumani Chande baada ya Rais magufuli kuondoka eneo hilo.
Jaji, Othuman akikagua gwaride lililokuwa limeandaliwa baada ya rais kuondoka.
Zoezi la ukaguzi wa gwaride likiendelea.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewawakia mahakimu, majaji na ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka hapa nchini (DPP) kuharakisha kesi zote zilizopo mahakamani ambazo hazihitaji kufanyiwa uchunguzi, zitolewe hukumu mara moja.
Hayo ameyasema leo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama (Siku ya Sheria) iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Posta jijini Dar es Salaam ambapo alipokea hotuba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyosomwa mbele yake pamoja na hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande.
Baada ya kupokea hotuba hizo, Rais Magufuli amekubali kufanyia kazi hotuba hizo, likiwemo suala la ukosefu wa fedha za marekebisho ya ujenzi wa mahakama chakavu zilizopo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Hata hivyo, aliwataka mahakimu, majaji na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kumuunga mkono katika kuhakikisha jitihada anazozifanya za kutumbua majipu nao watumbue ili kuendana na kasi yake.
Amesema hakuna haja ya Mkurugenzi wa Mashtaka, pamoja na polisi kutumia kauli ya kuwa ‘uchunguzi bado unaendelea’ ametaka kauli hiyo kupuuzwa na kuachwa mara moja akisema mtuhumiwa hasa mwenye uthibitisho kamili kesi yake ihukumiwe mara moja hata kama itakuwa siku moja baada ya tukio husika.
“Kama mtu anakamatwa na pembe za ndovu kwani kuna haja gani ya kusema kuwa uchunguzi unaendelea?” Alihoji rais na akaamuru hukumu ichukuliwe papo hapo mahakamani anapofikishwa mtuhumiwa.
Rais Magufuli aliwapongeza majaji wote walioonesha kwa kipindi cha mwaka jana walionekana kuharakisha kesi zaidi ya 900 na akidai wote hao waongezewe mishahara yao huku akilia na waliochelewesha kutoa hukumu za kesi kwamba wachukuliwe hatua mara moja tofauti na alivyokuwa amewapa siku saba za kujieleza.
NA DENIS MTIMA/GPL
Naiunga Mkono Kauli ya raisi kwani mtu ameshikwa na kizibiti uchunguzi unaendelea wanini?