MAGUFULI AZINDUA NYUMBA ZA ASKARI MKOANI GEITA (PICHA +VIDEO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora watatu kutoka kulia, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Wabunge pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani wa Geita.

RAIS John  Magufuli  leo amezindua nyumba 15 za makazi ya askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumiwa na askari 30. Akiongea na katika uzinduzi huo, amelipongeza Jeshi la Polisi na wizara husika kwa kutekeleza kwa makini mradi huo kikamilifu.

Katika hotuba yake ya uzinduzi huo, ametoa onyo kwa askari wanaowabambikia watu kesi na wanaokula rushwa, akiwataka kuondoka katika jeshi hilo na pia amevipongeza vyombo vya usalama na ulinzi kwa kusimamia amani nchini.

“Navipongeza vyombo vyote vya usalama na ulinzi kwa kusimamia suala la amani katika nchi yetu; endeleeni kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.  alisea rais na kuongeza: “Nakupongeza Mheshimiwa Kangi Lugola kwa kuwachukulia hatua askari 157 waliokuwa wakifanya kazi jeshini bila kufuata maadili ya kazi.  Vilevile  askari mtakaopata nafasi ya kuishi kwenye nyumba hizi mzitunze ili zidumu.”

Rais alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa madini ya dhahabu kuyatumia masoko ya dhahabu katika kuuza bidhaa zao hizo badala ya kuuza kwa madalali pembeni.

“Tumeanzisha masoko ya dhahabu, yatumieni;  msiuze dhahabu kwenye masoko yaliyofichika…  Msiwauzie walanguzi, hii itaisaidia serikali kujua kiasi kilichouzwa kwa ustawi wa uchumi wetu na maendeleo ya nchi yetu,” alisema na kuwataka  wananchi kwa jumla kujikita katika kudumisha amani nchini kwa ajili ya maendeleo.

Matukio katika Picha:


Loading...

Toa comment