The House of Favourite Newspapers

Magufuli gumzo Kanda ya Ziwa!

0

MAGUFULI (3)
Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufu.

Richard Bukos, aliyekuwa Geita

Dk John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa gumzo kubwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

magufuli bukoba mjini (2)Dk. Magufuli ambaye amekuwa ‘homa kali’ kwa vyama vya upinzani, aliingia mikoa ya Kanda ya Ziwa akitokea mkoani Kigoma ambapo alianzia Wilaya ya Chato mkoani Kagera kabla ya kuelekea mjini Bukoba na maeneo mbalimbali ambako alizua gumzo kwa sera na ahadi alizotoa kwa wananchi.

Katika ziara hiyo, wananchi walimpokea kwa shangwe, vifijo huku wakionesha hisia zao wazi jinsi ambavyo wanaamini Dk. Magufuli atafufua upya mwanga wa matumaini kwa wananchi katika nyanja mbalimbali.

wakazi wa wilaya mpya ya kyerwa walimiminika kwa wingi kusikiliza sera za magufuli leo (2)Mbali na wingi wa watu waliojitokeza kumlaki na kumsikiliza Dk. Magufuli, wengi walionekana kuvutiwa na aina ya sera ambazo mgombea huyo amekuwa akizinadi kwa uchambuzi na maelezo yanayojitosheleza jambo ambalo liliamsha ari ya shamrashamra kila mahali ndani ya mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa ambako alifika.

MAGUFULI TARIME (4)Wananchi wa maeneo mbalimbali katika kanda hiyo wamesema, Dk. Magufuli amekuwa hajipambanui kwa kuegemea chama chake (CCM), bali anatanguliza maendeleo ya nchi kwanza ndipo mambo mengine ya vyama yafuate.

Mara kwa mara, watu walisikika mbele ya mwandishi wetu wakisifu ahadi za Dk. Magufuli ambazo kwa hakika zimeonekana kutekelezeka na kuwagusa moja kwa moja wananchi wa hali zote za kimaisha.

Miongoni mwa ahadi ambazo zimegusa na kukonga nyoyo za wakazi wengi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, ni pamoja na kuboresha usafiri wa majini kwa kuongeza vyombo vya usafiri kwa njia hiyo mfano meli, feri na pantoni, ambazo ni tegemeo kubwa kwa wakazi hao kwa usafiri kutokana na mikoa hiyo kuzungukwa na ziwa Victoria.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply