The House of Favourite Newspapers

Magufuli Hatoshiriki Kongamano la Nyerere

0
Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere.

Taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma zinazomualika Mhe. Rais katika shughuli za kumbukumbu ya Mwl. Julius Nyerere zinakumbushwa kutokutangaza ushiriki wa Mhe. Rais Magufuli katika shughuli zao mpaka zipate uthibitisho kutoka Ofisi ya Rais.

Taarifa iliyotolewa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hatakuwa mgeni rasmi katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama inavyotangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

 

Leave A Reply