The House of Favourite Newspapers

Magufuli – “Kenyatta Kanipigia Simu, Corona Imepungua, No Lockdown”

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 20, 2020 amezungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali waliokuwepo njiani wakimsubiri alipokuwa akipita akitokea Chato Mkoani Geita akielekea Jijini Dodoma.

Baadhi ya vitu alivyovisema Magufuli leo

“Ndugu zangu wa Singida, tuna tatizo la Corona, nikawaomba Watanzania tuombe, napenda kuwathibitishia Mungu ametusikia na janga hili limepungua sana pamoja na kwamba bado halijaisha, tuchukue hatua, hapa Singida wamebaki wagonjwa watatu wanaendelea vizuri”

“Corona ipo lakini naamini itaisha tu, lakini kikubwa tusiogope na wala tusitishane, hapa Singida naona hamjawa na hofu ndio maana waliovaa barakoa wachache, hata mimi sijavaa, Mkuu wa Mkoa pia hajavaa, tuombe Mungu, tuchukue tahadhari lakini tuchape kazi”

 

“Juzi nilipigiwa simu na Kenyatta nikiwa bado Chato, akanipa pole na kujielezea mambo ya Corona kidogo, leo pia mimezungumza naye pia, kuna kimgogoro kule mpakani mwa Kenya, Kenya ni marafiki zetu, Corona isiwe chanzo cha migogoro, sisi Marais tumeyamaliza.”

 

“Mimi na Kenyatta (Rais Uhuru) tumeongea kwenye simu tumeyamaliza, naagiza ndani ya wiki hii, Waziri wa Uchukuzi na timu yake wakakutane na waziri wa Kenya kule mpakani wakiwa na wakuu wa mikoa ya mipakani kama Mwanza, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga ili wajadiliane”

“Nchi yetu sasa inakwenda mbele sana, uchumi wetu unakua. Tanzania ni miongoni mwa nchi tano Afrika zenye uchumi unaokua kwa kasi, zamani hapakuwa hata na mataa hapa Singida na hayo ndiyo maendeleo kwa hiyo tuendelee kuchapa kazi,”

 

“Niliwaomba Watanzania tuombe kwa siku tatu na tukafanya hivyo, ndugu zetu Waislamu wanaendelea kuomba. Niwaambie kuwa sasa hili janga limepungua kwa kiasi kikubwa, nawaomba tuendelee kuchukua tahadhari,”

 

 

Leave A Reply