Magufuli Kuikabidhi Simba Kombe La Ubingwa

Kikosi cha timu ya Simba.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar, mchezo ambao Wekundu hao watakabidhiwa kombe lao.

 

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambao Simba wataingia uwanjani wakiwa tayari mabingwa na hata kama wakifungwa bado watapewa kombe lao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.

 

Simba ilitangaza ubingwa huo wiki iliyopita baada ya wapinzani wao Yanga kufungwa na Tanzania Prisons kabla ya wao kuwafunga Singida United siku inayofuata.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia alisema tayari wamemuandikia barua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ya kumwalika Rais Magufuli kuhudhuria kwenye hafla hiyo.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia

“Tunatarajia Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi wa mechi kati ya Simba na Kagera na ndiye atakayekabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa ligi Simba kama ratiba yake haitabadilika.

 

“Kikubwa tunataka kuweka historia katika soka tena katika uongozi wetu mpya ulioingia madarakani TFF kwa kumwalika rais kuwa mgeni rasmi na kukabidhi kombe kwa mabingwa hao,”alisema Karia.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment