The House of Favourite Newspapers

Magufuli, Lowassa wazua balaa

0

Na waandishi wetu

WAKATI zikiwa zimesalia siku 35 kuelekea uchaguzi mkuu, kwa nyakati tofauti wagombea wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamezua balaa kufuatia watu kugombana baada ya kutofautiana kwa hoja za ushabiki, Risasi Jumamosi limesheheni matukio motomoto.

Katika tukio la awali, maeneo ya Mbagala- Charambee, jijini Dar mapaparazi wetu waliokuwa kwenye mizunguko yao, waliwanasa vijana waliosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema na CCM wakizichapa baada ya kubishana kuhusu wagombea hao wa urais.

“Ukitaka nikutoe damu basi itaje vibaya CCM miye nilikuwa nachambua sera za Magufuli wakatokea hawa jamaa wa Chadema, badala ya kutoa sera wao wanaleta ushabiki maandazi na kunitukana ndipo nikashidwa kujizuia. Baada ya kuanza kunishambulia kwa mateke ndipo na mimi nikajibu mapigo,” alisema kijana huyo wa CCM aliyejitambulisha kwa jina la Coco Byanco.

Katika tukio lingine chanzo chetu kilipenyeza picha za vijana wawili, wakazi wa Vingunguti, jijini Dar nao wakizichapa katika kibanda cha kuuzia magazeti baada ya kupishana kwa hoja kati ya Magufuli na Lowassa.

“Nimewapiga picha jamaa wawili wakizichapa katika kibanda cha magazeti. Kuna jamaa anaitwa Shalukan wa CCM, alikuwa anawaambia wenzake kwamba Lowassa hafai kuwa rais kwa sababu ni fisadi, jamaa wawili wa Chadema wakamvaa kwa maneno ndipo zikaanza kupigwa hadi walipotokea wasamaria wema kuwaamua,” kilieleza chanzo chetu huku kikimtumia picha mwandishi wetu kwa njia ya WhatsApp.

Tukio lingine katika kijiji cha Uvinza, mkoani Kigoma, wamama wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, walijikuta wakizichapa walipokuwa waking’ang’ania kukaa karibu na Magufuli aliyekuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa mkoa huo.

“Huyu dada bonge alikuwa mbele karibu kabisa na jukwaani alipo Magufuli, sasa huyu mwenzake mwembamba akawa haoni si ndiyo akajisogeza mbele ya huyu bonge ndipo mtiti ulipoanzia, kila mmoja akawa anataka kukaa mbele, wakazipiga kwelikweli hadi watu walipowaamua,” alieleza dada mmoja aliyeshuhudia ugomvi huo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply