Magufuli na siri ya Alhamisi

Gladness Mallya

SIRI nzito! Imebainika kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ana siri nzito na siku ya Alhamisi kwani matukio yote muhimu na makubwa yameonesha kujitokeza kwake ndani ya siku hiyo.

Akizungumza na gazeti hili juzi, mtaalamu wa mambo ya nyota nchini, Maalim Hassan Yahya alisema Dk. Magufuli ana siri nzito na siku ya Alhamisi ambayo inaonesha mambo mazuri kwake na nchi kwa ujumla.

Alieleza kwamba, siri hiyo inaanzia mwaka huu ambao unatawaliwa na nyota ya Mshale na Samaki, ulianza siku ya Alhamisi (Januari Mosi), kutangazwa kwake Dk. Magufuli kuwa rais pia ilikuwa siku ya Alhamisi (Oktoba 29) ambayo pia ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa.

Mbali na Alhamisi hizo, lakini pia utafiti unaonesha hata mwaka huu utaisha siku ya Alhamisi hivyo kuongezea usiri mkubwa wa siku hiyo kwa Rais Magufuli.

Kama hiyo haitoshi rais huyo aliapishwa siku ya Alhamisi (jana) ambapo inaonesha katika uongozi wake utakuwa wa mafanikio, wananchi maisha yao yatabadilika kwani kiongozi huyo ameonekana kuwa ana nyota kali.

“Uongozi wa Dk. Magufuli utakuwa mzuri sana maana nyota zimeonesha na hata malaika wanaotawala siku ya Alhamisi ambayo imeonesha kuwa na matukio mengi kwake ni wazuri hivyo Watanzania watarajie Tanzania mpya yenye neema,” alisema Maalim Hassan.


Loading...

Toa comment