The House of Favourite Newspapers

Magufuli selema selema Mbeya, Njombe na Iringa

0

mafinga iringa (2)

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli, akiwahutubia wananchi wa Iringa, leo.
Magufuli akisalimiana na John MaleccelaMagufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, John Malechela.magufuli akizungumza na wakazi wa kijiji cha lujewa jimbo la mbalaliMagufuli akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Lujewa jimbo la Mbalalimwanjelwa mbeyaWananchi wa Mwanjelwa mkoani Mbeya wakimsikiliza Magufuli.soweto mbeya Wananchi wa Soweto mkoani Mbeya wakimsikiliza Magufuli.
vicheko vilinoga katik ya magufuli na maleccelaVicheko vilinoga kati ya Magufuli na Maleccela.wakaz wa chimala wakisikiliza sera za magufuliWakaz wa Chimala, Mbalali, mkoani Mbeya wakisikiliza sera za Magufuliwakazi wa chimala, mbalali mbeyaAkina mama wakazi wa Chimala, wakimshangilia Magufuli.wakazi wa makambako wakimsiliza magufuli hayupo pichaniWakazi wa Makambako wakimsiliza Magufuli hayupo pichani.mafinga iringa (1)Magufuli akizungumza na wakazi wa Mafinga, mkoani IringaJohn Malecela akiwasisitiza wakazi wa Kijiji cha Lujewa kumchagua magufuli kwa maendeleoJohn Malecela akiwasisitiza wakazi wa Kijiji cha Lujewa kumchagua Magufuli kwa maslahi ya Taifa.Abbas Kandoro naye aliibukia Kijiji cha Lujewa na kumsalimia MaleccelaMkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro naye aliibukia Kijiji cha Lujewa na kumsalimia Maleccela.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk Jonh Pombe Magufuli leo amepaa kwa ndege kutoka Kanda ya Ziwa na kufanikiwa kufika mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa ambako alifanya mikutano ya kampeni zaidi ya kumi kwenye maeneo tofauti ya ya mikoa hiyo.

Akifanya mikutano ya kampeni mkoani Mbeya, Magufuli aliwaahidi wakazi wa Wilaya ya Mbalali ambao wanasumbuliwa na tatizo la mgogoro wa ardhi kuwa, endapo atachaguliwa kuwa rais atatumia sheria namba 4 ya mwaka 1999 kuwatetea na kuwarudishia ardhi yao iliyochukuliwa na mwekezaji.

Akiwa ukanda huo huo, pia Magufuli aliwaomba wakazi wa maeneo hayo wampe kura ya urais ili nao awatetee warudishiwe eneo lao la vijiji 21 lililochukuliwa na TANAPA warejeshewe eneo lao ili waviendeleze vijiji hivyo.

Magufuli alisema kuwa, rais ndiye mwenye mamlaka na ardhi hivyo ataweza hata kutumia mamlaka yake kuwarejeshea eneo lao.

Alipofika eneo la Lujewa lilipo Wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya alikutana na Makamu wa Rais Mstaafu, John Malechela ambaye nae aliwaomba wananchi wa kijiji hicho kumchagua Magufuli na kuwaacha waroho wa madaraka waliokihama chama hicho baada ya kukosa nafasi nono za kuvuna mapesa.

PICHA NA STORY: RICHARD BUKOS/GPL MBEYA

Leave A Reply