Kampeni za Dk Magufuli zatua Geita
Wakazi wa Mji mdogo wa Katoro wilayani Chato, mkoani Geita wakisikiliza kampeni za Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Jonh Pombe Magufuli, leo.
Wakazi wa Katoro wakifurahia kampeni za Dk. Magufuli.Wakazi wa Kijiji cha Lulenge wilani Ngara, wakionesha kumkubari Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Jonh Magufuli.Wakazi wa Kijiji cha Nyakaula wilayani Ngara wakimsubiri Dk. Magufuli.Kundi la waimbaji wa muziki, Yamoto Band wakiwaburudisha wakazi wa Geita kwenye mkutano wa Kampeni za Dk. Magufuli uliofanyika, leo.
Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Jonh Pombe Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda mkoani Geita leo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Jonh Pombe Magufuli, leo alifanikiwa kuingia Mkoa wa Geita baada kumaliza kampeni zake mkoani Kagera.
Miongoni mwa maeneo aliyofanya mikutano hiyo leo ni pamoja na Vijiji vya Lulenge, Bukililo, Bugalama, Magamba, Mluzagamba, Nyakaula, Lunzewe vyote vya wiloayani Ngara mkoani Kagera.
Baada ya kuingia mkoani Geita, Dk Magufuli alifanya mikutano ya kampeni Vijiji vya Bwanga, Buselesele, Katoro na kumalizia Geita Mjini.
Dk Magufuli aliwaahidi wakazi wa Geita na Katoro kuwa, endapo watamchagua kuwa rais wa Tanzania, ataondoa kero za wakazi hao kufukuzwa maeneo ya migodi, kuboresha miundombinu na utendaji wa migodini, kuweka utaratibu utakawawezesha wachimbaji wadogowadogo kunufaika na migodi hiyo, kuondoa kero za maji, kuongeza barabara za lami sehemu mbalimbali alizopita na kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwaza mpata kidato cha nne.
Kesho alhamisi, Magufuli anatarajiwa kuelekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuwania urais wa Tanzania.
PICHA NA STORI: RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKO GEITA