The House of Favourite Newspapers

Maguri bado anawaota Tambwe, Kiiza

0

Elius-Maguli11

Straika wa Stand United, Elias Maguri.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam.

LICHA ya kuachwa kwa mabao sita na kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Hamis Kiiza wa Simba, straika wa Stand United, Elias Maguri, hajakata tamaa na bado anakiota kiatu cha dhahabu.

Kiiza ana mabao 16 akifuatiwa na Amissi Tambwe wa Yanga aliyefunga mabao 15 huku Jeremiah Juma wa Prisons na Donald Ngoma wa Yanga wakiwa na mabao 11 kila mmoja. Maguri ana mabao 10.

Tambwe & Busungu

Amissi Tambwe wa Yanga akishangilia na wachezaji wenzake.

Tangu kuingia mwaka huu, Maguri amefunga bao moja tu wikiendi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu na kuiwezesha timu yake kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Maguri ambaye alikuwa akiwekwa benchi na kocha wake Patrick Liewig kwa maelezo ya kujiona staa, alisema anaamini ndani ya mechi sita atakuwa anaongoza kwa mabao.

kiiza-akishangilia-baada-ya-kutikisa-nyavu-uwanja-wa-taifa-dar-es-salaam_f9e7nzxc6j531t6oujg70lpkp

Hamis Kiiza wa Simba.

“Nimeanza kucheza sasa, namuomba Mungu anipe afya njema niendelee na kasi yangu ya ufungaji niweze kuwaacha Tambwe na Kiiza ambao waliniacha baada ya kupata matatizo na kocha.

“Najua haitakuwa kazi nyepesi lakini nitapambana vilivyo kuhakikisha nawaacha na ikiwezekana mpango huo uweze kutimia ndani ya mechi zetu sita za ligi,” alisema Maguri aliyewahi kucheza Simba.

Leave A Reply