The House of Favourite Newspapers

Mahakama Kuu Yaahirisha Kesi ya Mdee na Wenzake 18 hadi Septemba 02 Mwaka

0

 

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha Kesi ya Mdee na wenzake 18 hadi Septemba 02 mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mawakili wa Wabunge hao kuwasilisha mapingamizi mapya mbele ya Jaji Syprian Mkeha kuomba Mahakama isianze kusikiliza shauri hilo mpaka pale pangufu ya kisheria yaliyojitokeza kwenye kesi hiyo yatakapotatuliwa.

 

Leo Mahakama ilitarajiwa kusikiliza shauri hilo ambapo upande wa Mawakili wa CHADEMA unoangozwa na Peter Kibatala walitarajiwa kuwahoji Wabunge nane kati ya 19.

 

Hii ni mara ya kwanza Kwa Halima Mdee na wenzake 18 kufika mahakamani hapo ambapo awali walikuwa wakiwakilishwa na Mawakili wao, Julai 29 mwaaka huu Mahakama iliahirisha kesi hiyo ambapo leo ilitarajia kuanza kusikiliza shauri la msingi.

WACHINA WAMFANYIA KUFURU MANZOKI WAMPA BILL. 1.4, YANGA WAJA NA MBINU MPYA CAF |KROSI DONGO

Leave A Reply