The House of Favourite Newspapers

Mahakama ya Juu Kenya Kutoa uamuzi wa kesi  ya Urais Leo Jumatatu

0
Majaji wa Mahakama ya juu Kenya

MAHAKAMA ya juu kenya leo inatoa uamuzi kulingana na kesi iliyo funguliwa na Raila Odinga ya kupinga matokeo ya urais baada ya kuonekana kuwa Dkt William Ruto amepata kura za kuwa  rais mteule wa kenya kutokana na kura zilizo pigwa Agost 9, 2022.

 

Endapo Majaji wanao simamia kesi hiyo wata tupiliambali malalamiko ya Raila Odinga na kukubaliana na matokeo yaliotangazwa na baraza la uchaguzi, Rais mteule William Ruto ataapishwa Septemba 13,2022 na kuwa rais wa awamu ya tano wa kenya na kuwa mrithi wa Uhuru Kennyatta.

Dkt william Ruto

Lakini kama hawata pitisha matokeo ya William ruto na kubatilisha ushindi wake na kuunga mkono mKesi iliyo funguliwa na  aliekuwa mgombea wa nafasi ya urais Raila Odinga basi mamlaka zitakuwa na siku 60 za kufanya uchaguzi mpya na kumpata rais ambae atashinda kihalali.

 

Raila Odinga

Imeandikwa: leocardia charles kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply