Mahakama ya kijeshi Uganda Yapigwa marufuku kusikiliza kesi za kiraia
Mahakama ya juu nchini Uganda imeamuru kesi zote zinazowahusu raia katika mahakama ya kijeshi zisitishwe mara moja kusiskilizwa na zihamishwe hadi mahakama za kawaida.
Jopo la majaji saba wakiongozwa na Jaji mkuu Alfonse Owing Dollo limeamua kwamba mahakama ya kijeshi imeundwa kisheria lakini ina uwezo tu wa kusikiliza kesi zinazowahusu wanajeshi na wala sio raia.
Majaji wamesema kwamba hakuna uhakika kwamba mahakama za kijeshi ni huru kutekeleza kazi yake kisheria kwa sababu majaji wa mahakama hiyo ni wanajeshi na wameteuliwa na rais.
Uamuzi huo ni ushindi mkubwa kwa watetezi wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakipinga hatua ya raia kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kijeshi.