The House of Favourite Newspapers

Mahakama Kisutu Yatoa Dhamana kwa ‘Video Conferencing’

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu  jana Januari 14, 2020,  kwa mara ya kwanza ilitoa dhamana kwa mahabusu Abubakari Seguni aliyekuwa katika Gereza la Keko kwa njia ya kimtandao maarufu kama ‘Video Conference’ ambaye aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya rushwa na uhujumu uchumi.

Dhamana hiyo ilitolewa na mahakama hiyo kwa kushirikiana na Gereza la Keko wakati ilipokuwa ikiendesha mashauri maane kwa njia ya hiyo ikiwa ni mwendelezo.

 

Mtuhumiwa huyo namba tatu  anakabiliwa na tuhuma hizo katika shauri namba 43 la mwaka 2017 la jinai, akiwa na wenzake watano dhidi ya serikali. Shauri hilo liletwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Awali Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali, Bi. Ester Martin,  alidai kuwa shauri hilo halijakamilika upelelezi wake na linasubiri kibali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Leave A Reply