The House of Favourite Newspapers

Mahakama ya Kisutu Yatupilia Mbali Ombi la Meya Mwita

0

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita kutaka mahakama hiyo kutoa amri ya kuzuia kikao cha kumvua cheo chake hicho.

 

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa, Januari 10, 2020 na hakimu Mkazi, Janeth Mtega ambaye amesema  kuwa Wakili wa Isaya Mwita hakufuata baadhi ya vigezo katika kufungua madai yake.

 

Hakimu Mtega amesema mahakama haiwezi kuzuia Meya huyo kuondolewa kwenye nafasi yake kwa sababu hakuna uthibitisho wa uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani wala hasara atakayoipata endapo akiondolewa.

“Mahakama hii inatupilia mbali hoja za kutaka muombaji (Mwita) kubaki madarakani kwa sababu hoja za Wakili wa muombaji hazina miguu ya kusimamia,” Hakimu Mtega.

 

Baada ya Hukumu hiyo, Isaya Mwita, amesema; “Nakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kwamba haiwezi kuzuia Meya huyo kuondolewa kwenye nafasi yake lakini nasisistiza kwamba mimi bado ni Meya wa Dar, na Jumatatu nitaenda kuomba gari kwa DED.

“Hata kama jana wangepiga kura 17 bado wasingeweza kunitoa. Wanasema nina matumizi mabaya ya gari, nilikuwepo kwenye gari siku ile ya ajali, ilikuwa ‘police case” na dereva wangu alishtakiwa kwa mujibu wa sheria, kosa langu liko wapi? Gari lilitengenezwa kwa sababu ina bima,”

 

“Leo asubuhi nimeripoti ofisini japo mkurugenzi ananipa gari sijui shida nini hivyo nimemuandikia Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam aniletee gari kwa haraka mno. Nakusudia kuwashtaki wote waliohusika kufoji saini ya Diwani ambaye yupo nje ya nchi na mmoja wa washtakiwa Hawa atakuwa Kigogo mkubwa tu katika Jiji la Dar es Salaam.

Leave A Reply