The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yafuta Mashtaka Yote Dhidi Diane Rwigara na Mama Yake

 

Jaji Xavier Ndahayo wa Mahakama Kuu ya Rwanda amewafutia mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili mwanasiasa Diane Rwigara na mama yake Adeline Rwigara waliyokuwa wakituhumiwa kufanya uchochezi dhidi ya Serikali ya Rais Kagame na kughushi nyaraka.

 

Mahakama imefikia uamuzi huo jijini Kigali, leo Alhamisi, Desemba 6, 2018 na kusema kwamba imefanya uamizi huo kutokana na upande wa mashitaka kutokuwa na ushahidi wa kutosha na kwamba hawana hatia kwa sababu mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote.

 

Wawili hao walishitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka ambapo mwendesha mashtaka wa Serikali ya Rwanda alikuwa ameiomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela lakini Diane na mama yek walikana mashtaka hayo wakisema yana mlengo wa kisiasa.

 

Kikundi cha wajumbe wa Bunge la Congress la Marekani walishinikiza Rwanda kuondoa mashitaka hayo, lakini Serikali ya Rwanda ilijibu kwamba haishinikizwi na yeyote na kuomba vyombo vya sheria visiingiliwe.

 

Uamuzi huo ulikuwa wa mwisho kuhusu maombi ya upande wa mashitaka ya kuwapa kifungo cha miaka 22 jela katika kikao cha mwisho mwezi uliopita, huku upande wa mawakili wao wakipinga maombi hayo na kusisitiza wateja wao kuachiwa huru mara moja.

 

Waendesha mashtaka waliomba hukumu hiyo wakisema Diane Rwigara alihusika katika kughushi nyaraka wakati alipokuwa akikusanya saini za wafuasi wake wakati wa kutaka kugombea urais kama yalivyo masharti ya tume ya uchaguzi na kwamba kumekuwa na saini za wafuasi hewa baadhi wakiwa walifariki dunia na wengine wakiwa hawapo nchini.

 

Kadhalika Diane Rwigara na Mamake walishitakiwa kuchochea chuki na kusambaza uvumi kwa lengo la kuhamasisha umma kugoma dhidi ya utawala.

Uamuzi wa leo ulisubiriwa kwa hamu na gamu baada ya Diane Rwigara na mamake Adeline Mukangemanyi kukamilisha kesi hii wakiwa hawako kizuizini. Kwa mshangao wa wengi, mapema mwezi wa 10 mwaka huu mahakama ilichukua uamuzi wa kuwaachilia huru kwa dhamana ikisema sababu za kimsingi zilizosababisha kesi yao kusikilizwa wakiwa kizuizini hazipo tena.

 

Wao Wanakanusha mashtaka dhidi yao wakisema yalichochewa kisiasa hasa baada ya Diane Rwigara kujitokeza katika ulingo wa kisiasa,akipinga wazi sera za chama tawala na kutaka kugombea urais katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

BREAKING: MBOWE Afikishwa Mahakamani, Arudishwa GEREZANI!

Comments are closed.