The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yaipa Simba Siku 14, Kulipa Mil 77

0

 

BARAZA la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni, limetoa siku 14 kwa Klabu ya Simba kulipa kodi ya pango la ardhi inayodaiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kiwanja no. 226 block 1 kilichopo Bunju Dar es Salaam ambapo ndipo kuna Uwanja wa Simba Mo Arena.

 

Oda hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhe. Said Wambili, baada ya Wakili kutoka Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam, Johancen Chibanda kuwasilisha ombi la kutaka kukamata mali zilizopo katika kiwanja hicho ili kufidia deni wanaloidai klabu hiyo.

 

Wakili huyo awali akiwasilisha ombi hilo, aliliambia Baraza kwamba wamekuwa wakipeleka ankara za malipo ili Klabu ya Simba ifanye malipo, lakini hawapati mrejesho wowote.

Aliongeza kuwa, hata jana ambapo ilitolewa oda hiyo ndani ya Mahakama ya Kinondini, Dar ya kulipia ndani ya siku 14, hakukuwa na mtu yoyote kutoka Simba kusikiliza shauri hilo.

 

Baada ya kueleza hayo, Mhe. Wambili, amesema kupitia kanuni ndogo ya 23 ya baraza hilo, inaeleza kuwa ili kutekeleza oda hiyo ni lazima itoe siku 14 kwa mdaiwa aweze kulipia na kama mdaiwa akishindwa kutekeleza ndani ya muda huo, baraza litatoa oda kwa mamlaka husika ili kutekeleza agizo la kukamata mali zilizo ndani ya ardhi ya mdaiwa.

 

Inaelezwa kwamba, katika madai hayo, Simba inadaiwa zaidi ya Sh milioni 77 na laki tano.

NA DENIS MTIMA | SPOTI XTRA

Leave A Reply