The House of Favourite Newspapers

MAHAKAMA YAMZUIA MWANAMKE KUOLEWA NA MWANAMUZIKI

RIYADH (AFP) – MWANAMKE mmoja nchini  Saudi Arabia amejikuta akibwagwa na mahakama katika dhamira yake ya kuolewa na mtu ampendaye, kwani mahakama imesema “kidini” mwanamme huyo hafai kwa vile hucheza chombo cha muziki, limesema gazeti moja la nchini humo jana.

Nchi hiyo ya kifalme na ya kihafidhina, huwataka wanawake kupata ruhusa kutoka kwa “walezi” wa kiume — baba zao, waume zao na jamaa wengine wa kiume — ili kuweza kusafiri, kuolewa na majukumu mengine.

Katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo, mwanamme anayecheza chombo cha muziki huonekana kuwa wa hadhi ya chini na mwenye sifa mbaya.

Pamoja na vikwazo kadhaa kama hivyo, Saudi Arabia, ambayo ni rafiki mkubwa wa Marekani,  imeanzisha mabadiliko kadhaa yenye kulenga kusafisha taswira ya nchi hiyo ya kifalme, ikiwa ni pamojana kuruhusu wanawake kuendesha magari.

Lakini bado inashutumiwa kwa kukumbatia mfumo wa wanaume kuwaamulia wanawake mambo mengi.

Comments are closed.