Mahakama Yapiga Chini Pingamizi la Serikali, Sasa Rufaa ya Mbowe Kusikilizwa

JAJI Rumanyika wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Ijumaa, Novemba 30, 2018 imetupilia mbali pingamizi la Upande wa Jamhuri la kuzuia rufaa ya dhamana iliyokatwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko isisikilizwe na hivyo imeamua kusikiliza rufaa hiyo leo kuanzia saa nane mchana.

 

Mbowe na Matiko wamekata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya hati ya dharura wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo.

 

Walifutiwa dhamana na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, anayesikiliza kesi hiyo Novemba 23 kutokana na maombi ya upande wa mashtaka yaliyodai wameshindwa kuhudhuria mahakamani wakati kesi yao ilipopangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali bila sababu za msingi.

 

UPDATES:

Upande wa Serikali umekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya dar es salaam kukubali kusikiliza rufaa ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko leo.

HATARI! Ulinzi Waimarishwa Mahakama Kuu/Rufaa Ya Mbowe, Matiko

Toa comment