The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yashindwa Tena Kutoa Hukumu ya Maxence Melo

0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa mara ya nne imeshindwa kutoa Hukumu juu ya kesi namba 456 inayomkabili Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo baada ya Hakimu anayeendesha shauri hilo kutokuwepo.

 

Hii Leo kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Thomas Simba. Melo anakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi na kuharibu uchunguzi kinyume na sheria.

 

Awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 ikapangwa tena kutolewa Disemba 06, 2019; baadae ikapangwa kutolewa Jan 22, 2020 kisha ikapangwa kutolewa leo Feb 19, 2020. Sasa itasomwa Aprili 2, 2020.

 

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu mkazi Huruma Shaidi hadi Aprili 2 mwaka huu. Ikumbukwe Melo alipandishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake Desemba 16, mwaka 2016.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply