Mahakama Yasogeza Mbele Uamuzi dhamana Ya Boniface Jacob wa Chadema
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Oktoba 1, 2024 imetupilia mbali maombi ya Serikali yaliyowasilishwa wiki iliyopita juu ya kiapo cha ziada kupinga dhamana ya mgombea uenyekiti Kanda ya Pwani, Boniface Jacob.
Hakimu Kiswaga alijaribu kurejea kesi kadhaa ambazo waleta maombi walileta kiapo cha ziada yaani Supplementary affidavit ambacho ni kiapo chenye maelezo ya ziada kufafanua zaidi juu ya kiapo cha awali na wala sio ushahidi
Hakimu Kiswaga alifanya kurejea kesi iliyokuwa mahakama kuu kati ya Ali Kombo na Hospitali ya Osterbay kiapo cha ziada kiliwekwa bila ruhusa ya mahakama na baadae jaji wa mahakama kuu alikitoa kiapo hicho kwa kuwa hakikufuata utaratibu.
Septemba 26, 2024 palikuwa na mchuano mkali kutoka upande wa utetezi na upande wa waleta maombi ambapo upande wa waleta maombi ulileta kiapo cha ziada ambacho ulikiwasilisha kupitia mtandao wa mahakama. Lakini upande wa utetezi ulisimama ukipinga kiapo cha ziada wakiiomba mahakama kutokupokea kiapo hicho kwani hakikufuata utaratibu wa kufaili viapo mahakamani.
Licha uamuzi huo Mahakama imesogeza mbele uamuzi juu ya dhamana mpaka tarehe 07 Oktoba 2024.