The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yatoa Maamuzi Kuhusu Nabii Tito

MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili (Mirembe), mkazi wa Kijiji cha Nong’ona, Onesmo Machibya maarufu kama (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili au la.

 

Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, amesema anahitaji majibu hayo Machi 5, mwaka huu siku ambayo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ikiwa ni baada ya agizo la kupimwa akili kutotekelezwa hapo awali.

 

 

Nabii Tito Machibya alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kupitia mafundisho anayoyatoa na amekuwa akiieleza mahakama kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kutoa vithibitisho kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili.

Comments are closed.