The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yatupa Madai ya Kubaka Dhidi ya Rambo

Image result for Sylvester Stallone

MWIGIZAJI maarufu wa Marekani, Sylvester Stallone,  hatafunguliwa mashitaka ya kubaka miaka karibu 30 iliyopita.  Habari hiyo imejitokeza baada ya mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Sly, kufungua  mashitaka akisema alibakwa mwaka 1987 na 1990.

 

Hata hivyo, Stallone ameyakana madai hayo. Ofisi ya mwendesha mashitaka ya L.A. County ilisema haitamfunguliwa mashitaka mwanamke huyo ambaye mashahidi aliowataja  walishindwa kuthibitisha madai hayo.

 

Licha ya mashitaka hayo kupitwa na wakati wa kupelekwa mahakamani, polisi wa Santa Monica, bado waliendelea na uchunguzi wa jambo hilo. Kwa upande wake, Stallone amemshambulia aliyemshitaki kwa kumfungulia mashitaka kwamba alisema uwongo katika hati ya mashitaka hayo. Hata hivyo, kesi hiyo imefungwa.

Comments are closed.