Waliomuua Khashoggi Waondolewa Adhabu ya Kifo

 

MAHAKAMA nchini Saudi Arabia imeondoa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu watano waliopatikana na hatia ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwaka 2018, vimesema vyombo vya habari.

 

Waendesha mashitaka wamesema wahusika walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya familia ya Khashoggi ambaye alikuwa ni mwaandishi wa habari kuamua kuwasamehe. Hata hivyo, mchumba wake amesema uamuzi uliofanywa ni “ni kejeli dhidi ya haki”.

 

Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji maarufu wa serikali ya Saudia aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Ufalme wa Saudia katika mji mkuu wa Uturuki, Instanbu,l na maafisa wa ujasusi wa Saudi Arabia.

 

Serikali ya Saudia ilisema kuwa mwandishi huyo wa habari aliuawa katika “operesheni ambayo haikukusudiwa ” na mwaka uliofuatia Saudi Arabia iliwashitaki watu 11 mahakamani kuhusiana na kifo hicho.

Toa comment