The House of Favourite Newspapers

Maharusi Wakesha Uwanja wa Mpira kwa Kukiuka Masharti ya Corona

0

Picha na video za bibi na bwana harusi wakiwa pamoja na familia zao zimepigwa wakiwa wamekesha katika uwanja wa mpira katika siku ya harusi yao kwa kukiuka masharti dhidi ya kujikinga na corona. Jambo ambalo limesababisha raia wengi wa Rwanda kukosoa kitendo hicho.

 

 

Polisi katika mji mkuu wa Kigali nchini Rwanda walisitisha harusi tatu katika sikukuu za pasaka kwa kosa la kukiuka masharti yaliyowekwa dhidi ya corona ya kukataza sherehe na kuwa na kikomo cha watu 20 pekee cha wageni wa kwenye harusi.

 

 

“Bibi harusi kukesha kwenye uwanja wa mpira usiku wote wa siku ya harusi yake ni kumbukumbu mbaya sana na haiwezi kusahaulika katika maisha yangu”, bibi harusi asema.

 

 

“Ni maumivu yasiyoelezeka na kudhalilisha watu kiasi hiki hakuwezi kutufanya kuiogopa corona au kufuata masharti yaliyowekwa ” – aliiambia BBC.

 

 

Msemaji wa polisi ameviambia vyombo vya habari kuwa kuna watu wengine zaidi wanafanya sherehe na kukiuka masharti yaliyowekwa dhidi ya corona na polisi hawataruhusu haya yaendelee.

 

 

Baadhi ya watu wamekosoa tukio hilo katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa wamevuka mipaka na hakuna sheria inayosema watu inabidi wazuiliwe usiku mzima , wengine walisifia hatua hiyo dhidi Covid ili kuhakiksha wanakuwa salama.

 

 

Clarisse Karasira, mwanamuziki kutoka Rwanda ameandika katika kurasa yake kuwa umekosa utu na kuongeza kuwa ni jambo linaloleta machungu kwa wapenzi hao waliokuwa wameoana.

 

 

Rwanda imesifiwa kimataifa kwa jinsi inavyokabiliana na janga la virusi vya corona lakini wanaharakati wameikosoa kwa kukiuka haki za binadamu katika hatua wanazozichukua kuhakikisha jitihada hizo zinafanikiwa.

 

 

Rwanda imerikodi zaidi ya watu 22,000 waliopata virusi vya corona na vifo 311 vilivyosababishwa na virusi hivyo.

Leave A Reply