MAHINDI HAYACHOMWI KWA GESI

KAMA nak-uona shoga yangu ulivyobetua macho juu kama unaangalia mkungu wa ndizi mbivu, utashanga sana na mwezi dume ndiyo huo unaelekea katikati! Hee heeeiyaaa wanasemaa nyakati za usiku hata konokono anaweza kung’ata, upo nyonyo?

 

 Hakuna kitu ninachokichukia kama mtu kusema eti mapenzi hela kifua kikubwa nenda kawe mlinzi, aliyekwambia mwanaume anapendewa kifua nani? Kashinde huko gym uone kama pesa itakufuata? Unajifanya mjanjaaa wakati una thamani ya kopo la chooni hadhi yako chooni kabatini ufuate nini? Wareee reeeee!

 

Shoga leo limenifika hapa hadi mwenzako nashindwa kuandika, tangu lini mgomba ukachanjwa kuni? Hivi jamani hadi tumeanza mwaka mpya bado kuna watu hawajui kumpikia mume? Shuuuutuuuu! Wanakwambia mapenzi mawasiliano, ukimya peleka maktaba! Shoga nimepokea meseji nyingi kutoka kwa wasomaji wengine wakinitakia heri ya sikukuu na wengine wakinipa malalamiko yao kwa kuuanza mwaka vibaya. Kuna mmoja amenifanya hadi nikasema siwezi kuliacha hivihivi acha niwachambe wote wenye tabia hizi.

 

Wakati mwingine sisi wanawake huwa sijui tunajisahau au akili zetu tumeshikiwa na aliyezishika ameshatangulia mbele ya haki, maana wakati wengine wanalia kutokuwa na bahati ya kuolewa wengine wanaipata na kuichezea! Kuna msomaji wa kiume amenitumia meseji ya kulalamika kuwa amefunga ndoa mwis-honi mwa mwaka jana na kabla ya hapo haku-wa aki-ishi naye hivyo hakuj-ua kiundani baadhi ya vitu.

 

Anasema mara baada ya ndoa amegundua kuwa mkewe hajui kupika chakula na kutokana na kulelewa kwa wazazi wake kumemfanya aishie kujua kutengeneza chai na kama atapika wali basi tegemea maji mengi, haloooo eeehhh nicheke miye kama mazuri! Hivi jamani dunia hii kuna wanawake hawajui kupika? Siku hizi hadi mitandao imejaa inakufundisha vyakula vyote kuanzia kukoleza mkaa hadi kuipua chakula napo umeshindwa? Chefuuuu!

Shoga wanakwambia chafya ya mpishi haizimi moto na mahindi hayachomwi kwa jiko la gesi, umeolewa shikamana mama usije kuchekwa na mawifi mwishowe ukaachika! Mwanamke hata uwe mrembo vipi, wowowo vipi lakini kama hujui kupika shoga sawa na kabati tu ndani ya nyumba kutwa linawekewa vyombo tu!

 

Ifike mahali tuwe tunawaonea hata huruma waume zetu shoga, siyo kila siku vyakula vya kununua na ukibahatika kidogo unapika tambi na chapati loooh! Kwa mwezi huu kama hujui kupika na mumeo pesa mpaka mwisho wa mwezi unategemea mnaishije humo ndani?

 

Mwanamke usiishie ujanja sita kwa sita, ujanja wa kucheza na feni na kubadilisha staili, mwanamke kuwa mjanja wa mikono kama unaweza kuitumia kwenye sita kwa sita basi iweze kuitumia na jikoni, upo nyonyo? Nisiwe muongeaji sana shoga yangu, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri! Ni mimi Shangingi Mstaafu Anti Naa.

 

Loading...

Toa comment