Mahujaji waliokufa, ambao hawajarudi

ahamed said bawaziri (tanga) kafaAlhaj Ahamed (kafa).

Na Makongoro Oging’

Baadhi ya wananchi ambao ndugu zao walikwenda kuhiji mjini Mina, Maka, Saudi Arabia, wana hofu kwa kuwa asilimia kubwa bado hawajarejea nchini huku wengine wakitajwa wamefariki dunia.

hadija shekari mohamed (dar) kafaHajat Khadija (kafa).

Wananchi hao waliohojiwa na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa nyakati tofauti walisema ni mahujaji wachache waliorejea, wengine wamefariki dunia na kuzikwa huko na baadhi hawajaonekana kabisa huku kukiwa na taarifa kuwa wapo wanaotarajiwa kurudi hivi karibuni.

athuman mateso chaulani (pwani) kafaAlhaj Athuman (kafa).

Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda ofisi ya taasisi mojawapo inayosafirisha mahujaji ijulikanayo kwa jina la Ahlu Daawa Hajj iliyopo Magomeni jijini Dar na kukutana na mmoja wa viongozi, Ustadhi Yusuph Mohamed ambaye alikuwa na haya ya kusema:

fatia mohamed karim (tanga) hajarudiHajat Fatia (hajarudi).

“Ni kweli tumepokea taarifa ya vifo vya mahujaji na kuna wengine wanaendelea na matibabu huko huku baadhi yao wamesharudi na wapo ambao tunatarajia kuwapokea Oktoba 10, mwaka huu, najua kila mmoja anajua kilichotokea huko, mahujaji wengine bado hawajulikani walipo.

zuhura toba waziri  (tanga) hajarudi

Hajat Zuhura (hajarudi).

“Tutaendelea kutoa taarifa kadiri tunavyopata habari kwani tumekuwa tukiwasiliana na uongozi wa taasisi hii ambao wako huko Maka na tuna ushirikiano na ubalozi wetu wa huko na Wizara ya Mambo ya Nje ya hapa kwetu ambao wamekuwa nasi bega kwa bega kufuatilia suala hili,” alisema Ustaadhi Mohamed.


shafi ally (dar) kafa

Alhaj Shafii (kafa).

Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Seif Salum Kitimla, Shafi Ally, Hadija Shekari Mohamed wote wa Dar, Ahamed Said Bawazili waTanga na Athumani Mateso Chaulana wa Pwani.

joha salim baraka (tanga) hajarudi

Hajat Joha (hajarudi)

Aliwataja mahujaji waliorudi, walipotoka kwenye mabano kuwa ni Salama Jumbe Mkumbo (Pwani), Badilu Abdallah Kiboko (Bukoba), Abdallah Mwidadi Kuluvya (Tanga), Seleman Salum Said (Pemba), Rehema Salehe Mbaraka (Tanga), Ramadhani Sharia Amir (Dar).

Aliwataja wengine kuwa ni Issa Ibrahim Magoye (Mpanda), Mohamed Seif Kiukala (Pwani), Fatina Mohamed Said (Dar), Haruna Yahaya Kiyekumbya (Karagwe), Mohamed Issa Kidomi (Dodoma), Mwanamkuu Mohamed Ahmed (Tanga) na Abdallah Mohamed Al Lawii (Zanzibar).

Alisema ambao bado hawajarudi ni pamoja na Hawesu Mashaka Mwinyimkuu (Dar), Idd Musa Kibadeni (Tabora), Masibu Mohamed Fikirini (Morogoro), Fatia Mohamed Karim (Tanga), Zuhura Toba Waziri (Tanga).

Wengine ambao hawajarudi ni Hirari Hamis Salum (Bukoba), Salim Nassoro Salim (Pemba), Joha Salim Baraka (Tanga), Sophia Abdallah Msindo (Tanga), Karim Fatia Ali (Pemba) na Siwatu Misho Mwishehe (Dar).


Loading...

Toa comment