The House of Favourite Newspapers

Mahujaji Wanne Watanzania Wafariki, Makka

0

mahujai (2)Miili ya mahujaji walikufa kwenye tukio hilo.mahujai (3)Miili ya mahujaji walikufa kwenye tukio hilo ikiwa imefunikwa.mahujai (1)

Muonekano wa umati wa mahujaji katika mji wa Makka.

Makka, Saudi Arabia

MAHUJAJI  wane Watanzania wamethibitishwa kufariki dunia katika tukio la kukanyagana lililotokea jana huko Mina katika mji wa mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia. Watanzania hao waliopoteza maisha ni miongoni mwa mahujaji 717 kutoka sehemu mbalimbali za dunia waliopoteza maisha na wengine zaidi ya 800 katika tukio hilo wakati wa siku ya mwisho ya Hija (jana).

Taarifa ya Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abu Bakari Zuberi iliyotolewa akiwa Makka imewataja watanzania watatu waliokwisha tambulika majina yao kuwa ni Bi. Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.

Mtanzania mwingine mwanamke aliyekufa jina lake bado halijatambulika, pia yupo raia mmoja wa Kenya Bi. Fatuma Mohammed Jama ambaye alisafiri Makka kwa kutumia wakala wa Tanzania.

Leave A Reply