The House of Favourite Newspapers

Maimartha Jesse Achonga Sura Yake

0
Mtangazaji wa wa Azam Televisheni, Maimartha Jesse.

STORI: HAMIDA HASSAN | RISASI | TANO KALI

MTANGAZAJI wa Azam Televisheni, Maimartha Jesse amefanya upasuaji wa kuchonga sura yake kitu alichokuwa akikiwaza kila siku kwani maisha ya akina Kim Kardashian na Black Chyna huwa yanamfurahisha.

Akizungumza na Risasi Jumamosi , Maimartha alisema kuwa kutokana na jinsi anavyopenda urembo ameamua kuchonga sura yake awe na muonekano wa tofauti na kueleza kuwa waliomshawishi kufanya hivyo ni Kim Kardashian na Black Chyna ambao huishi kwa kujibadili kila kukicha.

“Kiukweli kilichonivutia kuchonga sura yangu ni muonekano wa pua ya Kim Kardashian, najua yeye hufanya upasuaji wa mara kwa mara, kwa kuanza nimeanza na sura nimefanikiwa naamini nikitamani kurekebisha na kitu kingine nitafanya pia,” alisema Mai aliyedai kuwa anapenda urembo kuliko kitu chochote.

Leave A Reply