The House of Favourite Newspapers

Mainda awaomba radhi mashabiki

0

MaindaBrighton Masalu

KUTOKANA na kukaa kimya kwa muda mrefu bila kujihusisha na kazi yake ya uigizaji, msanii wa muda mrefu, Ruth Suka ‘Mainda’  amewaomba radhi mashabiki zake kwa kitendo hicho na kuweka wazi kuwa yuko ‘bize’ na mambo mengine nje ya sanaa lakini muda si mrefu atajikita tena kwenye kazi hiyo na kwamba mashabiki hao watarajie makubwa zaidi.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu katikati ya wiki hii, Mainda alisema, alipoamua kumtumikia Mungu kwa dhati, aliamua kuachana kwa muda na mambo mengine ya kidunia ikiwemo uigizaji, lakini kwa sasa atarejea kwa kishindo, hivyo mashabiki wasiwe na shaka yoyote juu yake.

“Niwaombe radhi mashabiki zangu, si kwamba nimeachana kabisa na uigizaji la hasha, unajua nilipoamua kumtumikia Mungu, niliweka kando kidogo mambo mengi ya kidunia ikiwemo uigizaji, lakini kwa sasa nitarejea na mashabiki watarajie vitu vizuri zaidi kutoka kwangu kwani Mainda ni yuleyule,” alisema msanii huyo.

Leave A Reply