MAISHA YA MTANDAO YAMPOTEZEA MUDA LYNN

Irene Charles ‘Lynn’

KWANI lazima? Socialite na video vixen anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva hasa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Irene Charles ‘Lynn’ amesema siku hizi haonekani kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu maisha ya mitandaoni yanampotezea muda. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Lynn alisema watu wengi sasa wamegundua kuwa maisha ya mitandaoni yanadanganya na kama mtu asipokuwa makini, hawezi kufanya chochote cha maana zaidi ya kudili na mitandao ya kijamii.

“Nilikaa na kuwaza kuhusiana na maisha ya mtandaoni maana yanaweza kukufanya ukawa bize bila sababu ya msingi hivyo hata ukiniona kwenye mitandao ni kwa sababu maalum tu,” alisema Lynn aliyeuza nyago kwenye Wimbo wa Kwetu wa Rayvanny.

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment