The House of Favourite Newspapers

Video: Maiti 7 za Mto Ruvu, Baba Aibuaka Adai ni za Watoto Wake (+Video)

Baadhi ya vijana na wazee wa Kijiji cha Mloka Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakiongea na waandishi wa Uwazi (hawaonekani Pichani).

STORI: ISSA MNALLY, RICHARD BUKOS | UWAZI

PWANI: Miezi miwili baada ya zile maiti saba za Mto Ruvu wilayani Bagamoyo mkoani hapa, mkazi wa Kijiji cha Mloka Wilaya ya Rufiji mkoani hapa, Baba, ambaye ni mzee Ally Kitimai ameibuka na kudai kuwa, wanaye watano, walipigwa risasi miezi miwili iliyopita na watu waliokuwa na bunduki kisha kuondoka na miili hivyo kutia shaka kuwa, huenda zile maiti zilizokutwa Mto Ruvu ni miongoni mwa watoto wake, Uwazi limechimba kwa kina.

Moja ya Maiti Saba iliyokutwa Mto Ruvu ikiwa imefungwa kwenye kiroba.

MAJINA YAANIKWA

Mzee Kitimai aliwataja vijana hao ambao wote ni wa kiume kuwa ni Nassoro Kitimai, Ramadhani Kitimai, Mohammed Kitimai, Mussa Kitimai na mtoto wa mdogo wake, Hassan Fundi ambapo alisema walipigwa risasi  wakiwa wanarudi kijijini kutoka kuvua samaki kwenye bwawa moja lililopo kando ya Mto Rufiji kwenye Hifadhi ya Pori la Wanyama ya Selous inayopakana na kijiji hicho.

MAITI ZACHUKULIWA

Alisema baada ya kuuawa, watu hao waliondoka na miili yote mitano ambapo hawakujua ilikopelekwa mpaka leo. Waliokuwa na marehemu hao na kufanikiwa kutoroka wakati wakishambuliwa, ndiyo waliotoa taarifa baada ya kurudi kijijini.

SIMULIZI YA BABA WA MAREHEMU HAO NI HII

Akizungumza kwa uchungu na Uwazi kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita, mzee Kitimai alisema: “Suala la sisi wanakijiji kuuawa kwa kupigwa risasi tunapokwenda kuvua samaki limekuwa la kawaida mpaka kuna kipindi wanakijiji tulishawahi kuandamana ili kufika kwenye kituo kimoja cha askari kilichopo karibu na kijiji hiki lakini tulipofika kwenye geti la kuingilia tulikuta askari hao wameweka bendera nyekundu na kutuonya kuwa atakayethubutu kukanyaga eneo hilo itakuwa ndiyo mwisho wa maisha yake.”

Inasikitisha

SIKU YA TUKIO LA WATOTO WATANO

Mzee Kitimai aliendelea kuweka Bongo Muvi, Bongo Fleva hakukaliki DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya askari, wafanyabiashara na wasanii wa filamu za Kibongo (Bongo Muvi) na wale wa muziki (Bongo Fleva) wanaodaiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, hali bado ni tete miongoni mwa wasanii wa tasnia hizo kila mmoja akiwa hajui hatima yake.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, hasa baada ya wote waliotajwa awali kuanza kushughulikiwa kikamilifu, umebaini kuwa wasanii wengi wamekuwa wakihofia majina yao kujumuishwa kwenye orodha hiyo, huku wengine wakilazimika kutimkia mikoani, kwenda kusikilizia upepo unavyoenda.

“Hali ni tete kaka, Dar es Salaam inawaka moto kwa sisi wasanii, sasa hivi matumbo joto maana huwezi kujua kama na wewe jina lako litaongezwa kwenye orodha au laa! Unajua sisi wengine ni wasafi kabisa lakini huwezi kujua, mtu anaweza kukutaja wazi kwamba, siku ya tukio la kuuawa kwa vijana hao, walikuwa wakitoka kuvua samaki kwenye moja ya mabwawa yaliyopo karibu na kijiji hicho.

Maiti nyingine kwenye kiroba

“Sasa wakiwa njiani kurudi nyumbani, walishtukia wakishambuliwa kwa risasi na watu waliokuwa na bunduki.Wanangu wote watano waliuawa palepale lakini kuna wenzao wawili waliweza kuponyoka na kufanikiwa kufika hapa kijijini na kutueleza kilichotokea.”

AFUATILIA MAITI

“Baada ya tukio hilo, niliona hata kama wanangu walikuwa na makosa mimi niliamua kumwachia Mungu, hivyo nilifuatilia miili yao kule walikopigiwa risasi ili niweze kuileta kijijini niihifadhi kwa mujibu wa dini yangu ya Kiislam lakini haikuwa rahisi kwani kufika eneo lile hatukuiona miili. Ina maana waliondoka nayo wenyewe baada ya kuwauwa.”

SI MARA YA KWANZA

“Mauaji haya kutokea si mara ya kwanza na staili yake ni hiyohiyo ya kutopata miili baada ya wenzetu kuuawa. Si kijiji hiki tu, kuna vijiji vingine jirani na sisi pia wamekuwa wakiuawa na miili wanaichukua. Sasa sijui wauaji huwa wanaipeleka wapi?” alihoji mzee huyo.

Akaendelea: “Hata kama hao watu wakiwakamata wanakijiji wakifanya jambo lolote ambalo ni baya kwao, kwa nini wasiwafikishe mbele ya vyombo vya dola badala yake wao wanaamua kuwaua? Mimi naona kuna siku hilo linaweza kusababisha hali kuwa tete, kuna siku na sisi hatutakubali.” Uwazi:

“Kuna wakati kule Bagamoyo, kwenye Mto Ruvu unapoingia Bahari ya Hindi iliokotwa miili ya watu watano, kesho yake mtu mmoja na siku iliyofuata tena, mtu mmoja, jumla wakawa saba. Je, huoni kama inaweza kuwa watu hao watano ni miongoni mwa watoto wako?”

TAARIFA ZA MIILI YA BAGAMOYO

Mzee Kitimai: “Bahati mbaya sana mimi nimechelewa kupata kwa sababu ya chuki zake tu na wewe ukaingizwa kwenye orodha,” alisema msanii mmoja wa siku nyingi kwenye Bongo Fleva kwa masharti ya kutotajwa jina lake baada ya kuhojiwa na mwandishi wetu. Jacob Stephen almaarufu JB, ni msanii wa filamu za Kibongo ambapo kwa upande wake, alifunguka:

MWANAKIJIJI MWINGINE.

Mwanakijiji mwingine aliyezungumza na Uwazi kijijini hapo, alisema anaamini miili ya watu watano iliyoopolewa Mto Ruvu miezi miwili iliyopita ni ya watoto wa mzee Kitimai pamoja na miili ya watu wengine wawili waliopigwa risasi kwenye eneo hilo na kwenda kutupwa kwenye mto huo.“Tukio la kuuawa kwa watoto wa mzee Kitimai na miili yao kuchukuliwa na wauaji, linahusiana kabisa na miili iliyoopolewa Mto Ruvu, ingawa taarifa hizo zilichelewa kufika huku kijijini. Halafu nataka mjue, si kijiji hiki tu.

Sehemu ya wanakijiji hao wakiwa wamemzungura mzee Kitimai

Kuna vijiji vingine vilivyo jirani na hapa pia wakazi wake wamekuwa wakipigwa risasi na kufa na maiti zao kutoonekana. “Tungepata taarifa mapema tungeenda kuitambua miili hiyo ingawa hata hivyo, ikibidi lazima huyu mzee akapime kipimo cha vinasaba (DNA) ili kujiridhisha kama ni watoto wake kweli au la,” alisema mwanakijiji huyo huku akikataa kutaja jina lake.

UWAZI OFISI ZA SERIKALI YA KIJIJI

Baada ya kuzungumza na wanakijiji hao ambao idadi yao ilifikia 40, Uwazi lilifika kwenye Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mloka na kukutana na Afisa Mtendaji wa Kijiji, Ally Rwambo ambaye alithibitisha kutokea kwa mauaji ya mara kwa mara ya wanakijiji wake wanapokutwa wakifanya shughuli mbalimbali kwenye eneo hilo. “Ni kweli hapa kijijini kumekuwa na mauaji ya mara kwa mara yanayofanywa na watu fulani wakiwa na sare hali iliyosababisha kipindi fulani wanakijiji tuandamane. Baada ya maandamano hayo yaliyoambatana na vurugu, tulikaa kikao viongozi wa kijiji na kuonesha msimamo wetu,” alisema Rwambo.

Afisa Mtendaji wa Kijiji, Ally Rwambo

Akaongeza: “Lakini pia tuliwahi kupeleka maombi yetu kwa uongozi wa Hifadhi ya Selous ili na wao watusaidie kupambana na watu hao kama wanaweza kuwapata, mauaji yakatulia. Lakini sasa naona kama yameanza tena.”

HIFADHI YA PORI YA SELOUS

Hifadhi ya Pori ya Wanyama ya Selous ambapo Mto Rufiji wanakovua samaki wanakijiji hao unapita, ndiyo kubwa kuliko nyingine zote nchini Tanzania. Hifadhi hii iko kwenye mikoa ya Lindi (Wilaya ya Liwale), Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma na Mtwara, Morogoro na sehemu ya Mkoa wa Pwani.   Hifadhi hiyo ni kama nyingine ambapo, askari wa mbuga wamekuwa wakipambana na majangili usiku na mchana ili kulinda wanyama ambao ni maliasili ya nchi.

TUMEFIKAJE HAPA?

Desemba, mwaka jana, maiti saba ambazo hazikutambuliwa zilikutwa zikielea kwenye  Mto Ruvu eneo la Bagamoyo mkoani Pwani tena zikiwa zimehifadhiwa kwenye mifuko ya sandarusi ‘viroba’ vyenye uzito wa kilo 200 huku zikiwa zimeharibika vibaya. Diwani wa Kata ya Makurunge, Paul Kabile aliwaambia wanahabari kuwa, maiti hizo ambazo zote zilikuwa za jinsia ya kiume, ziligunduliwa na wavuvi waliokuwa wakifanya shughuli ya uvuvi kwenye mto huo.

Alisema maiti 5 kati ya hizo, ziligunduliwa Desemba 6, mwaka jana, majira ya alfajiri kwenye Kitongoji cha Kitopeni wilayani Bagamoyo, ambako wavuvi hao waligundua miili hiyo wakati wakiendelea na shughuli zao za uvuvi kwenye mto huo.

Alisema maiti 5 ziligunduliwa Desemba 6, alfajiri na nyingine moja iligunduliwa kesho yake, Maiti hizo, alisema kila moja ilikuwa imehifadhiwa kwenye kiroba huku zikiwa zimewekewa mawe na mifuko hiyo ikiwa imeshonwa juu kama vile yamehifadhiwa mahindi au mchele. Wavuvi hao baada ya kuziona maiti hizo walizizika kutokana na kuharibika sana na kushindwa kuzipeleka hospitali kwa hifadhi.

Wanakiji wakiwa kwenye mkutano na viongozi wao (hawapo pichani), kulia ni mwandishi wa Gazeti la Uwazi, Richard Bukos.

SIKU CHACHE BAADAYE

Baada ya kuibuka kwa maswali juu ya maiti hizo ambapo pia iliongezeka moja na kufikia 7, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kupitia kituo kimoja cha runinga nchini, alisema huenda miili ya watu hao saba waliokutwa kwenye mto huo ni wahamiaji haramu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lilithibitisha kuonekana kwa maiti hizo na kueleza kuwa, linafanya uchunguzi kwa kushirikiana na daktari ili kufahamu watu hao walikufa kwenye mazingira gani. Hata hivyo, mpaka sasa, hakujawahi kutolewa tamko lolote la kuonesha kuwa, maiti zile zilikuwa ni za akina nani!

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ACP Bonaventura Mushongi

KAMANDA WA POLISI AULIZWA

Ili kupata undani wa habari hii, Uwazi juzi lilimpigia simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ACP Bonaventura Mushongi na kumuuliza kuhusu madai ya mzazi huyo ambapo alisema: “Nipo mahali, nipeni muda kidogo nitawapigia mimi.”

Mpaka Uwazi linakwenda mitamboni, Afande Mushongi hakupiga simu na alipopigiwa tena yeye, hakupokea.

Gazeti la UWAZI Toleo la Februari 7, 2017

UWAZI NA UONGOZI WA SELOUS

Baada ya Kamanda Mushongi, Uwazi likampigia simu kiongozi wa Selous Kituo cha Mtemele kilichopo karibu na kijiji hicho, Mohammed Nyenye (Mudy) ili kumuuliza kama wanakijiji hao wamewahi kupeleka maombi ya kuomba msaada wa kuwasaka watu wanaodaiwa kuwaua wanavijiji hao kwa risasi, ambapo alisema yuko jijini Dar kwa matibabu na kumtaka mwandishi awasiliane na bosi wake aliyemtaja kwa jina la Lora Meikoki, naye alipopigiwa simu alisema yuko Sengerema mkoani Mwanza na hana taarifa hizo. “Mimi nipo huku Sengerema, Mwanza, lakini sina taarifa zozote,” alisema Meikoki

           Video: Maiti 7 za Mto Ruvu, Baba Aibuaka Adai ni za Watoto Wake

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.