The House of Favourite Newspapers

Maiti Yapotea Mochwari Ndugu Wagoma Kuendelea na Mazishi Mpaka Wapate Mwili wa Marehemu

0

 

FAMILIA moja katika kaunti ya Makueni nchini Kenya imelazimika kuahirisha hafla ya mazishi ya ndugu yao baada ya kuwepo kwa madai ya kupotea kwa maiti.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na familia ya Waema Nguku (95) ndugu hao walishtuka baada ya kuona mwili waliopewa na Hospitali ya Rufaa ya Makueni, kuwa siyo wa ndugu yao

Tukio hili lilizua kizazaa na kuleta hali ya sintofahamu baada ya ndugu hao kurudi hospitalini hapo siku ya Ijumaa Septemba 16, 2022 kufuatilia mwili wa ndugu yao ambao haukuonekana siku ya Alhamisi Septemba 17, 2022 na kuambiwa wachukue mwili mwingine tofauti na mwili wa ndugu yao.

“Baada ya kushindwa kutuonyesha mwili wa baba yetu, tuliondoka na kurejea siku ya Ijumaa ili kufuatilia lakini tulipofika Mmoja wa wasimamizi wa hospitali hiyo alituambia tuchukuwe mwili mwingine ambao siyo wa baba yetu lakini tulikataa,” alisema Kamene Waema ambaye ni motto wa mwisho wa marehemu.

Ndugu hao Wanasema walikuwa tayari wamenunua jeneza la mzee huyo na kuelekea makafani Alhamisi, Septemba 15, 2022 kuchukua mwili wake ambapo walikuwa wamepanga kumzika mzee huyo siku ya Jumamosi, Septemba 17, na matayarisho yalikuwa yamekamilika na hata kaburi lake lilikuwa tayari limechimbwa lakini walilazimika kuahirisha kutokana na hali hiyo ya sintofahamu iliyojitokeza.

Msimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Makueni, Joseph Masila alisema kwamba suala hilo linachunguzwa ili kutambua ni familia ipi ilipewa mwili usiokuwa sawa.

Aidha, moja ya familia iliyozozika ndugu yao wiki iliyopita, imethibitisha kuwa ilipewa mwili usiokuwa sawa na kuutambua kama wa Mzee Nguku, hivyo kufuatia ripoti hiyo, familia ya Nguku sasa inasubiri ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Rekodi za hospitali hiyo zinaonyesha kuwa miili 12 ilichukuliwakwa wiki iliyopita ambapo maiti tano zilikuwa za wanaume.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply