The House of Favourite Newspapers

Majabvi amfunika mshahara kocha Simba SC

0

majadviMzimbabwe Justice Majabvi.

Hans Mloli, Dar es Salaam

MUDA mwingine cheo si ishu sana kama unaingiza pesa nyingi zaidi ya bosi, ndivyo inavyotokea kwa sasa Simba SC baada ya mchezaji wa kimataifa wa timu hiyo, Mzimbabwe Justice Majabvi kuvuta mkwanja mrefu mwisho wa mwezi zaidi ya bosi wake mpya, Mganda, Moses Basena.

Imeelezwa kwamba tayari Simba imeshaelewana kila kitu na kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda iliyotwaa Kombe la Chalenji juzi Jumamosi na anatarajiwa kutua rasmi nchini leo Jumatano kuja kuanza kazi.

Basena aliyewahi kuinoa Simba miaka ya nyuma kwa vipindi viwili tofauti, anatarajia kurejea kwa mara nyingine, safari hii akiwa kocha msaidizi akirithi mikoba ya Selamani Matola aliyetimkia Geita Gold Sports.

Moja ya vitu ambavyo wameelewana na kuafikiana ni katika suala la mshahara ambapo Simba imemuahidi kumlipa Basena dola 1,500 (zaidi ya Sh milioni 3) kwa mwezi, ikiwa ni tofauti ndogo na mshahara anaouchukua Uganda wa dola 1,000 (zaidi ya Sh milioni 2,000,000).

Lakini uchunguzi uliofanywa na Championi Jumatano umebaini kuwa Majabvi anachukua mshahara ‘mrefu’ zaidi ya kocha huyo, ambapo kwa mwezi anachota dola 2,000 (zaidi ya Sh milioni nne).

“Basena tayari tumemalizana naye katika masuala ya mshahara, tumekubaliana kumpa dola 1,500 kwa mwezi. Tulikuwa tunasubiri amalize majukumu yake ya Chalenji na timu ya taifa, kwa hiyo sasa atakuja Jumatano hii,” kilisema chanzo kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Leave A Reply