The House of Favourite Newspapers

Majadiliano Serikali, Barrick Gold Yaanza

0
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais. John  Magufuli kujadiliana na uongozi wa Barrick Gold Corporation akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza  mazungumzo hayo leo  jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu madini yanayochimbwa  na kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar es Salaam.

 

Prof. Kabudi akiwaelekeza jambo.

 

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa,  imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.

 

Prof. Kabudi akiwa na wageni hao.

 

Profesa Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya nchi ipasavyo.

Prof. Kabudi akipata picha ya pamoja na ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo.

 

Imeelezwa Williams ameshukuru uwepo wa majadiliano hayo akisema Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande zote mbili.

Prof. Kabudi akizungumza akiwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni hiyo, Richard Williams,  kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo.

 

Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za kamati zingine mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na nyingine ya kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga huo unaosafirishwa nje ya nchi.

Leave A Reply