The House of Favourite Newspapers

Majaliwa kuongoza harambee ujenzi Shule ya KKKT inayogharimu Sh1.9 bilioni Mwanza

0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kassim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Imani Kanisa Kuu.

Mradi wa ujenzi wa Shule hiyo ambao umeshaanza katika eneo la Buswelu wilayani Ilemela mkoani Mwanza unagharimu Sh1.9 bilioni huku ukiwa umefikia zaidi ya asilimia 40.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Mwanza, Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Imani Kanisa Kuu, Andrew Gulle amesema ujenzi wa shule hiyo unalenga kutimiza matakwa ya Umisionari unaohimiza dini kuwagusa waumini kiroho, kimwili na kiakili.

Askofu Gulle amesema harambee hiyo itafanyika Jumapili Aprili 16,2023 KKKT kuanzia Saa 4 asubuhi huku akiwataka wananchi kutoka imani zote kujitokeza katika ibada na harambee hiyo.

“Kazi ya Kanisa ni kufanya injili kamili (Holistic Mission) ya kumgusa mwanadamu kimwili, kiakili na kiroho, kwa hiyo kujenga kanisa ni utume wa kumgusa mwanadamu kiakili ambapo watoto wa kitanzania na wasiyo wa Tanzania watapata fursa ya kukombolewa kifikra,” amesema Askofu Gulle

Askofu Gulle amesema ujenzi wa shule hiyo ambayo itakuwa na majengo mbalimbali yakiwemo majengo mawili yenye ghorofa tano yatakayotumika kama Hosteli za wanafunzi wa jinsi zote, madarasa, jengo la chakula, Utawala na majengo mengine unaendelea vizuri huku ukitegemea harambee hiyo kukamilika.

 

Leave A Reply