Majaliwa: Michezo Ni Nyenzo Muhimu Inayodumisha Amani
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano katika michezo ni nyenzo muhimu katika kudumisha diplomasia na amani miongoni mwa nchi washirika wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM).
Amesema hayo leo Ijumaa, Mei 17, 2024 wakati akifunga Mkutano wa 79 wa Baraza hilo. Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Johari Rotana jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amwmwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.