Majaliwa: Nimefurahishwa na Utekelezaji wa Agizo la Rais Dkt. Samia
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa amefarijika kuona Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwadhibiti Tembo wanaovamia mashamba na makazi ya wanananchi kwenye wilaya za Nachingwea, Liwale na Ruangwa katika mkoa wa Lindi.
Amesema hayo leo (Desemba 2, 2022) wakati alipopewa taarifa ya zoezi hilo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Elbate Mjingo kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea mkoani Lindi.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Samia alipohutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Desemba 01, 2022 kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuwatumia watalaamu wake kutekeleza agizo la kuwadhibiti tembo wanaovuka mipaka ya hifadhi na kuvamia makazi na mashamba ya wananchi.
Vilevile, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza kamati za ulinzi na usalama kwenye wilaya hizo kutoa elimu kwa wananchi juu ya utekelezaji wa zoezi hilo ikiwa pamoja na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ili kutosababisha wanyama kurudi kwenye maeneo ya makazi na mashamba.