WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Iringa akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Ally Salum Hapi kufika ofisini kwake jijini Dodoma Januari 7, mwaka huu, kumweleza sababu za kuzuia nguzo za umeme kusafirishwa mkoani humo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme katika vijiji vya mikoa ya Nyanda za Kusini.
Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akihutubia mkutano wa hadhara Kijiji cha Nyoni Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
“Halmashauri za Mufindi na Iringa wamezuia nguzo za umeme, wanataka posho, wanataka zilipiwe kodi, nimeagiza tarehe 7, saa tano asubuhi, waje ofisini kwangu Dodoma. Wananchi wanasubiri umeme wao wamezuia nguzo wanasubiri posho, wanaidai serikali wakati na wao ni serikali,.. Tutakutana ofisini.
“Waziri wa Tamisemi, aambatane na wakuu wote wa wilaya zilizozuia, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi, Mkuu wa Wilaya ya Iringa na Waziri wa Nishati. Sisi tumeahidi umeme kwa wananchi wanyonge wao wanazuia, wafike ofisini kwa waziri mkuu, waniambie kwa nini wanazuia,” alisema Majaliwa.
Comments are closed.