The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Tuchukue Tahadhari ya Corona, Tupige Nyungu

0

WAZIRI Mkuu, Kassimu Majaliwa amewasisitiza Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona. Amewataka waendelee kuzingatia mambo ambayo yanayosaidia kupunguza maambukizi ikiwemo kujifukiza nyungu, kunywa juisi ya tangawizi na malimao pamoja na kufanya mazoezi.

 

Majaliwa ameyasema hayo leo Julai 21, 2021 wakati wa ibada ya Sikukuu ya Eid Al Adha iliyofanyika katika Msikiti wa Mtoro jijini Dar es Salaam. Amesema ugonjwa upo nchini hivyo ni lazima Watanzania kujua umuhimu wa kujikinga pamoja na kuomba Mungu aepushe na ugonjwa huu.

 

“Tunao wagonjwa wachache tuendelee kuwaombea jukumu la Serikali ni kutoa huduma kwa wanaofikwa na ugonjwa huu, lakini pia tusiache kujikinga,”

 

“Tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, pamoja na kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko. Pia tuendelee kujikinga kwa kufanya mazoezi, juisi yetu ile tusiiache, lakini pia kukaa kwenye joto ambapo tuliipa jina la nyungu nayo itumike ili kupambana na ugonjwa huu,” amesema.

 

Kuhusu chanjo, Waziri Mkuu amesema amesema ipo na kwamba anayetaka akachanje kwani tayari hospitali zimeelezwa mahali.

 

“Tumesema kuchanja ni hiari, hivyo kama unataka kuchanja nenda mahali zilipo. Kama unaona umuhimu mwakani kwenda Hijja, una watoto wanasoma nje ya nchi na hairuhusiwi kwenda mpaka uwe umechanjwa basi fursa ipo hapa hapa usiangaike kwenda nje,” amesema.

Leave A Reply