The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Watanzania Wanatamani Timu Zao Zifanye Vizuri

0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Watanzania wanatamani kuona timu zao za Taifa za michezo mbalimbali zinafanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

 

Amesema kuwa uwezekano wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 ni mkubwa kutokana na matokeo mazuri ambayo imeyapata katika michezo ya minne ya awali.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba Mosi, 2021) wakati wa kikao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, uongozi wa TFF pamoja na wadau wa mpira wa miguu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

“Tukifanikiwa kushinda mechi hizo mbili zilizobaki kati ya timu ya Taifa na Congo pamoja na mechi ya timu ya Taifa na Madagascar ambayo itachezwa ugenini, itatupa matumaini ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia, hivyo Serikali inaamini ushirikiano kati ya wadau na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni muhimu katika kufanikisha lengo hilo.”

Waziri Mkuu amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema anatamani kuona timu ya Taifa soka ya wanaume (Taifa Stars) inafanya vizuri kama ilivyo kwa timu ya Taifa ya soka wanawake ambayo hivi karibuni ilichukuwa ubingwa kwenye mashindano ya kombe la COSAFA 2021 yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Leave A Reply