The House of Favourite Newspapers

‘Majambazi’ 7 Yanaswa Dar, Pia Bastola na Risasi 9 – Video

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam liimefanikiwa kukamata bastola aina ya FATIN 13- TURKEY yenye namba T.0622010J00535 ikiwa na risasi tisa ndani ya magazine huko maeneo ya Tangi-Bovu Mbezi.

 

Taarifa ya polisi inasema tarehe 04/07/2019, majira ya saa nne na nusu usiku kikosi maalum cha kuzuia na kupambana na majambazi kilifanikiwa kumkamata Michael Nina@Stellu (27) Mkazi wa Tangi-Bovu akiwa na silaha hiyo ambayo inasadikiwa kutumika katika matukio ya kihalifu maeneo mbalalimbali ya jiji.

 

Katika mahojiano na Jeshi la Polisi mtuhumiwa anakiri kupewa silaha hiyo na mwenzake ambaye hamfahamu kwa jina ila anamtambua kwa sura na jina moja la “Mama mdogo”. Jitihada za kumtafuta mtuhumiwa huyo zinaendelea.

 

Wakati huohuo, watu saba wanaohisiwa kuwa majambazi wamekamatwa wakiwa na Bajaj mbili zinazohisiwa kuwa za wizi, na vifaa vingine mbalimbali, vyote hivyo vikiwa vimepatikana maeneo ya Ukonga jijini hapa.

 

Watuhumiwa hao ni Said Salum (27), Amo Kefas (30), Said Ahmad (38), Mohamed Musa (31), Mboke Samwel (26), Abdallah Kipaneli (25) na Mfaume Mussa (25).

 

Taarifa inasema, mnamo tarehe 9 Julai 2019,  majira ya saa nane usiku huko maeneo ya Kibeberu na Magole ,Ukonga,  watuhumiwa hao walivunja maduka matatu na kufanikiwa kuiba bidhaa mbalimbali zikiwemo fedha  na Bajaj mbili zenye namba za usajili MC 312 CFB aina ya TVS na MC 540 CED aina ya TVS zote zikiwa na rangi ya bluu.

 

Baada ya wizi huo taarifa zilipokelewa katika kituo cha Polisi Stakishari na upelelezi ulianza mara moja ambapo mnamo tarehe 9 Julai 2019, majira ya saa tano asubuhi watuhumiwa walikamatwa huko maeneo ya Hondogo Gogoni Kiluvya wilaya ya Ubungo.

 

Aidha watuhumiwa hawa wamekuwa wakifanya matukio ya uhalifu kwa kutumia gari aina ya Toyota Harrier nyeusi yenye namba T.666 DJG ambayo inashikiliwa na Jeshi la Polisi ili kubaini mmiliki wake. Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

LAZARO B. MAMBOSASA – SACP

KAMANDA WA POLISI

KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

11.07.2019

#LIVE: KAMANDA MAMBOSASA ANAZUNGUMZA MUDA HUU

Comments are closed.