The House of Favourite Newspapers

Majambazi Yavamia Kanisa Katoliki Mbezi, Yapora Sadaka za Pasaka

WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia na kuvunja Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na vifaa vya kuendeshea ibada ya misa usiku wa kuamkia leo Aprili 5, 2018. Paroko wa Parokia hiyo, Sunil Kishor amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha na kusema, ambapo majambazi hao waliingia kanisani hapo na kuiba vitu hivyo, ikiwemo fedha za sadaka zilizokusanywa tangu Sikukuu za Pasaka hadi sasa.

 

“Nimepokea simu kuwa kuna hilo tukio la watu kuvamia kanisa hapo Mbezi, ni vibaka wameingia kanisani, wakaiba pesa na baadhi ya vitu. Pesa hizo zinaelezwa zilikuwa ni za sadaka tangu Sikukuu ya Pasaka japo thamani yake bado hatujafahamu kwa kuwa tukio ndiyo limeripotiwa muda si mrefu. Tunaendelea kufuatilia na tukipata taarifa kamili tutawaarifu, tunaendelea kulifanyia kazi”, amesema Mambosasa.

 

Aidha, Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuwabaini waliohu wa tukio hilo, ili kuwashughulikia ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Comments are closed.