Majanga! Familia Zatupiwa Vyombo Vyao Nje, Nyumba Yavunjwa

Familia zikiwa zimetupiwa vyombo nje.

MAJANGA! Jumla ya familia zipatazo saba wiki moja iliyopita zilijikuta katika wakati mgumu kufuatia kubomolewa kwa nyumba waliyokuwa wakiishi, kufuatia mke mdogo wa mmiliki wake, kufika na kubomoa jengo hilo baada ya kushinda kesi ya mzozo wa kifamilia mahaka­mani.

Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar


Tukio hilo la kusitikitisha lilitokea Septemba 5 mwaka huu huko Mtaa wa Mtongani Kunduchi jijini Dar ambapo familia hizo zilianza maisha mapya ya kupigwa na jua, mvua na baridi nje, huku baadhi yao wakipoteza mali na fedha kufuatia mama huyo kufika eneo hilo akiwa ameandamana na katapila na mabaunsa, bila hata kutoa notisi kwa wapangaji wake.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa mmiliki wa nyumba hiyo ambaye hivi sasa ni mare­hemu, aliyetambuliwa kwa jina moja la Robert, alisema mzozo wa kugombea mali hizo ulianza mara tu baada ya kufariki kwa baba yake aliyekuwa na wake wawili, huku mkubwa akiwa naye ametangulia mbele za haki.

“Baada ya kifo cha baba yetu, tulibaki na mama yetu mdogo, tukiwa jumla ya watoto watano, yeye aliishi kwenye mji wake akiwa na wanaye watatu, na mimi na mdogo wangu tukaba­kia kwenye nyumba hii (iliyobo­molewa) hata hivyo siku chache baadaye mama akatutaka tu­hame akidai nyumba hii ni yake aliachiwa urithi na baba yetu.

“Hatukuwahi kuwa na ugomvi wowote na mama yetu huyo, kwa kweli tulishangaa sana, tulipokataa akaamua kutupe­leka mahakamani, akisema eti tumemdhulumu mali za mumewe, mambo yale yalikwen­da harakaharaka mno, ukweli ni kwamba alitushindwa kesi, mali hizi akakabidhiwa yeye kama mwangalizi mkuu. Siku chache baadaye akatuletea ujumbe aki­tutaka tuhame akisema anataka kubomoa na kuuza eneo hili,” alisema Robert.

Vyombo vikizagaa nje.

 

“Baada ya nyumba kubo­molewa tumejikuta tukikosa pa kuishi, mali na fedha zetu zime­potea, usalama wetu na watoto wetu umekuwa mdogo mno, hadi sasa hatujui kesho yetu ni nini” alimaliza Godfrey.

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mama huyo aliyeju­likana kwa jina moja la Roda, lakini hakuweza kupatikana, in­gawa Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tabu Athuman, alikiri kuusikia mgogoro wa familia hiyo kwa muda mrefu.

ALLY KATALAMBULA, RISASI MCHANGANYIKO.

 

Wakazi wa Arumeru Wanavyotaabika na Ukame, Hali Inatisha!


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment