Kartra

Majembe Mawili ya Mtunisia Yarejea Yanga

UNAAMBIWA sasa ni rasmi majembe chaguo la Mtunisia wa Yanga, Nasreddine Al-Nabi, Abdalah Shaibu ‘Ninja’, na kiungo wao kipenzi Carlos Carlinhos, ambaye pia aliumia hivi karibuni hatimaye kwa pamoja wamerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa takribani wiki tatu wakiuguza majeraha ya nyama za paja.

 

Mbali na hivyo, Ninja na Carlinhos kwa pamoja walikosa mechi mbili za timu hiyo, ikiwemo ile ya Namungo ambayo Yanga ilicheza ugenini na kutoka suluhu kisha mbele ya JKT Tanzania ambapo walishinda mabao 2-0.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema, Ninja na Carlinhos wamepona na kwamba tayari wameshaanza mazoezi na walitarajiwa kuukosa mchezo wa jana dhidi ya Mwadui ambao ni wa Kombe la Shirikisho na wataendelea na mechi zingine za michuano ijayo.

 

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwajalia afya njema vijana wetu Ninja pamoja na Carlinhos na kubwa tumpongeze daktari wetu Nahumu Mganda kwa kusimamia matibabu yao vizuri.

 

Hadi muda huu wanafanya mazoezi yao chini yake, hivyo baada ya wenzao kurejea kwenye ligi wataungana tayari kwa kuwa sehemu ya msaada kikosini,” alisema Bumbuli

Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam


Toa comment