The House of Favourite Newspapers

Majeruhi Ajali ya Moto Moro, Watoka Muhimbili – Video

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imethibitisha kuwa, majeruhi watatu kati ya 11 wa ajali ya moto Morogoro waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo, wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya zao kuimarika.

 

Akizungumza leo Septemba 12, Dkt Edwin Mrema  ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Upasuaji amesema kuwa, kabla ya kuwaruhusu  hospitali hiyo imewapa huduma za kisaikolojia kwa kuwa tatizo la moto lilikuwa limewathiri kwa kiasi kikubwa.

 

Akizungumzia mgonjwa ambaye hadi sasa yuko kitengo cha uangalizi wa karibu (ICU), amesema kwa kuwa alikuwa ameungua zaidi miguuni, iliwalazimu kutoa viungo ambavyo vilionekana kupoteza uhai na amehifadhiwa katika chumba maalumu cha uangalizi ili kuzuia maambukizi kwa majeraha yake.

 

Aidha wakati mgonjwa mmoja bado yupo ICU, wengine wapo wodi ya kawaida wakiendelea na matibabu na hali zao zinaimarika.

 

Tukio la ajali ya moto Mkoani Morogoro, lilitokea Agosti 10, baada ya lori la mafuta kupinduka na kupelekea mlipuko huo ulioua zaidi ya watu 60 papohapo, ambapo hadi sasa vifo vya ajali ya moto huo vimefikia 104.

Comments are closed.